UDOMASA
University of Dodoma, Chimwaga Complex, P.O. Box 259,Udom, Cell +255 755 210310,
+ 255 713 004127, Email: udomasa2011@gmail.com
Ndugu zangu wanaudomasa, niwape hongera na pole kwa kazi za kila siku. Naomba niwajulishe yaliyojiri katika kikao cha Baraza (Council) kuhusu RUFAA za kina DOTTO:-
1. Katika kikao chake cha 23, Baraza la Chuo chini ya mwenyekiti wake Mh. Balozi Juma Mwapachu limetumia ubabe kukataa kupokea taarifa ya maamuzi ya kamati ya rufaa juu ya rufaa ya wafanyakazi waliosimamishwa kazi iliyosikilizwa tarehe 10/2/2012.
2. Hoja iliyopelekea maamuzi hayo ni kisingizio ya kwamba wakati wa kusikiliza rufaa menegimenti inadai haikutendewa haki kwa madai kwamba haikutaarifiwa kwa maandishi na hivyo basi haikuwakilishwa.
3. Baraza baada ya tuhuma hizo kwenye kikao cha jana ikaamuru rufaa hizi zisikilizwe UPYA ndani ya mwezi wa nne na kamati tendaji ya baraza itakaa kwa dharura tarehe 30/4/2012 kwa ajili ya kupokea taarifa ya kamati ya rufaa.
Ndugu wanaudomasa, kwa kuzingatia yaliyojiri katika kikao hicho; ni wazi kuwa hii ni hujuma, dhuluma, unyanyasaji na mwendelezo wa ukiukwaji na upokonywaji wa haki zetu.
Ukweli halisi ni kwamba menejimenti ilikuwepo, hii inathibitishwa na yafuatayo:-
A.Uwepo wa Mwanasheria wa chuo (Bw. Melkiory Sanga), Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala (Bi. Subira Sawasawa) na Afisa Mkuu wa Utawala (Bw. John Kusaja) katika vikao vyote vya rufaa, na kama wanakataa ya kuwa wao sio menejimenti, ni dhahiri kwamba wanatakiwa watuambie walienda kama nani? Na kutafuta nini katika vikao vya KAMATI HURU. Wakishindwa Kujieleza walienda kutafuta nini, inabidi hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao kwa kuvamia na kuvuruga shughuli za kamati huru ya rufaa.
B. Barua za kuwaatarifu walalamikaji juu ya kusikilizwa kwa rufaa zao ilitoka katika ofisi ya mwanasheria wa chuo. Hivyo swala la kutokuwa na taarifa sio la kweli kwa sababu kwa taratibu za kiutawala, lazima mwanasheria wa chuo alipata ridhaa kutoka kwa kiongozi wake wa kazi.
MWONGOZO-
Kwakuzingatia yaliyotokea-
1. kamati kuu ya UDOMASA imeshakaa na kushauriana na wanasheria na kutengeneza muongozo ambao unachanganua njia ambayo tutaelekea.
2. Tunatarajia kuitisha kikao cha dharura baada ya pasaka - ili tupeane miongozo zaidi juu ya hatua gani za kuchukua. Taarifa kamili za kikao hicho zitatolewa mapema wiki ijayo- baada ya UDOMASA ex-com kukaa jumatatu ya tarehe 2/4/2012.
1 comment:
JAMANI MANAGEMENT YA UDOM NI VC,DVCPFA NA DVCARC, WENGINE WOTE NI VIBARUA TU. KAMA KWELI HIZO THREE FIGURES HAZIKUPATA TAARIFA NI TATIZO. HAO WENGINE WATASEMA NINI WAKATI MABOSI WAO HAWANA TAARIFA. HATUNA JINSI ZAIDI YA KUWAFUATA WAO VILE WANAVYOTAKA. LAKINI WAKAE WAKIJUA HAKI YA BINADAMU HAIDHULUMIWI. ITAPATIKANA HAPA DUNIANI,NA MBINGUNI PIA. NI BORA WAITOE HAPA DUNIA MAANA MBELE YA MAHAKAMA YA MUNGU NI BALAA.
Post a Comment