Ndugu wana UDOMASA Salaam,
Poleni na majukumu ya kila siku. Pokeeni taarifa ya hatua zilizokwisha kuchukuliwa na UDOMASA juu ya ripoti ya maamuzi ya Rufaa amabayo ilikataliwa na Baraza la Chuo kaktika kikao chake cha tarehe 30/3/2012. Maelezo ya kina juu ya hatua hizo yanapatikana kwenye documents zilizoambatishwa kwenye e-mail hii.
Documenti hizo ni kama ifuatavyo:
1. Tamko la UDOMASA
2. Barua ya Kupinga hatua ya Baraza kukataa kupokea ripoti ya maamuzi ya kamati ya rufaa
3. Majibu ya Tangazo la PFA kuhusu makato ya 8% kwa wadeni wa HESLB
TAFADHALI DOWNLOAD NA MSOME
Pia tunatarajia kuitisha kikao wiki ijayo siku ya Jumanne tarehe
17/4/2012 ili kujadiliana na kuamua juu miongozo zaidi. Tutabandika matangazo na kuendelea kujulishana juu ya kikao hicho kwa njia mbalimbali. Tafadhali ukiona taarifa hii hakikisha unamjulisha mwingine. Tujiandae kwa ajili ya mkutano huo. Naomba sana tuhudhurie kwa wingi. Nawatakia kila la kheri katika utendaji kazi zetu za kitaaluma, kiutafiti na ushauri. Tafadhali tuzifanye kwa bidii na moyo wote.
Wenu,
Richard-Naibu Katibu wa Udomasa

No comments:
Post a Comment